NGULI wa zamani wa soka wa Ureno, Luis Figo amesisitiza Barcelona inaweza inaweza kumsajili Cristiano Ronaldo kama wakifanikiwa kutengua mkataba wa nyota huyo wa Real Madrd. Figo aliwahi kuondoka Barcelona na kwenda Madrid kufuatia klabu hiyo kutengua kitenzi cha mkataba wake ambacho kilikuwa kiasi cha paundi milioni 37.2 mwaka 2000 kipindi hicho ikiwa ada iliyovynja rekodi kwa mchezaji. Nguli huyo amesema jambo hilo linaweza kutokea hata wakati huu kwa Ronaldo kunyakuliwa na Barcelona kama wakiwa tayari kuweka fedha ezani. Ronaldo ambaye ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa Ulaya hivi karibuni kwa mara ya pili anatajwa kuwa na kitenzi cha euro bilioni 1.5 katika mkataba wake. Figo amesema sasa hivi wako katika soko huria hivyo kama klabu ikitokea na kutengua hicho kitenzi hakuna shaka kuwa lolote linaweza kutokea.

No comments:
Post a Comment