RAIS wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu amedai kuwa kwasasa klabu hiyo inaangalia uwezekano wa kumuongeza mkataba kipa wao Marc-Andre ter Stegen. Klabu hiyo tayari imeshatangza nia ya kuwaongeza mkataba nyota wake kadhaa akiwemo Lionel Messi, Luis Suarez na Ivan Rakitic katika miezi inayokuja. Na sasa Bartomeu amemuongeza Ter Stegen katika orodha, pamoja na nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 24 kuwa bado na mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo. Akihojiwa Bartomeu amesema wanafanya hivyo ili kuweka hali ya amani katika klabu hiyo na kutoa nafasi kwa wachezaji kuendelea kuifanya kazi yao kwa kujiamini zaidi.

No comments:
Post a Comment