NGULI wa zamani wa soka wa Arsenal, Gilberto Silva amekiri kuwa kazi yake mpya ya ukurugenzi wa soka katika klabu ya Panathinaikos ya Ugiriki ni ngumu kuliko alivyotegemea. Kiungo huyo wa zamani wa kimataifa wa Brazil, ambaye alikichezea kikosi cha nguli wa zamani wa Arsenal dhidi ya AC Milan Jumamosi iliyopita, ameteuliwa kushikilia wadhifa huo kiangazi hiki kufuatia kuichezea kidogo klabu hiyo mwaka 2008 na 2011. Kazi hiyo mpya wa Gilberto inamuhitaji kutafuta wachezaji wenye vipaji na kufanya majadiliano ya usajili kwa wachezaji wanaowahitaji. Akihojiwa Gilberto ambaye ana umri wa miaka 39 amesema ni maisha mapya na mazingira mapya kwake lakini ni jambo zuri linalomvutia kwani lina changamoto kubwa.

No comments:
Post a Comment