Tuesday, September 6, 2016

MAJERUHI MESSI AIPA KIWEWE BARCELONA.

KLABU ya Barcelona imethibitisha kuwa Lionel Messi bado ameendelea kusumbuliwa na majeruhi ya mtoki, lakini hakuna tarehe yeyote iliyopangwa ya kurejea uwanjani mpaka sasa. Klabu hiyo imegundua majeruhi hayo kabla Messi hajarudi Argentina kwa ajili ya mchezo wao wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Uruguay Alhamisi hii. Wiki iliyopita kocha wa Argentina Edgardo Bauza amesema hakukuwa na haja na kumtumia Messi kwa ajili ya mchezo wao wa leo dhidi ya Venezuela na sasa kuna hatihati ya kuukosa mchezo wa Barcelona dhidi ya Alaves mwishoni mwa wiki hii. Hata hivyo, pamoja na klabu hiyo kukiri Messi kusumbuliwa na mejaruhi hayo lakini wamedai bado anaweza kucheza katika mchezo dhidi ya Alaves.

No comments:

Post a Comment