Wednesday, September 7, 2016

FA KUMUUNGA MKONO VAN PRAAG UCHAGUZI UEFA.

CHAMA cha Soka cha Uingereza-FA kimetangaza kumuunga mkono rais wa Shirikisho la Soka la Uholanzi Michael van Praag katika uchaguzi wa rais wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA. Van Praag mwenye umri wa miaka 68, amekuwa akiliongoza Shirikisho la Soka la Uholanzi toka mwka 2008 na pia ni makamu wa rais wa UEFA. Katika kinyang’anyiro cha uchaguzi huo kitakachofanyika Septemba 14, Van Praag atapambana na rais wa Shirikisho la Soka la Slovakia Aleksander Ceferin. Akihojiwa mwenyekiti wa FA, David Gill amesema wanamuunga mkono Van Praag kwasababu wanafahamu atakuwa kiongozi imara. UEFA inatafuta rais mpya baada ya kiungo wa zamani wa Ufaransa Michel Platini kujiuzulu wadhifa wake huo Mei 9 mwaka huu baada ya kushindwa rufani yake kupinga kufungiwa kujishughulisha na masuala ya michezo.

No comments:

Post a Comment