Wednesday, September 7, 2016

KOCHA USWISI AMTETEA XHAKA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Uswisi, Vladimir Petkovic amemuunga mkono Granit Xhaka baada ya kiungo huyo wa Arsenal kutolewa nje katika mchezo walioshinda mabao 2-0 dhidi ya mabingwa wa Ulaya Ureno jana usiku. Xhaka mwenye umri wa miaka 23, alitolewa nje dakika ya tisini baada ya kulimwa kadi ya pili ya njano katika mchezo huo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia. Nyota huyo sasa anatarajiwa kukaa benchi katika mchezo ujao dhidi ya Hungary Octoba 7, lakini anaweza kurejea katika mchezo dhidi ya Andorra siku tatu baadae. Akihojiwa Petkovic amesema kadi mbili za njano alizopewa Xhaka zilikuwa nyepesi sana hivyo hadhani kama alistahili.

No comments:

Post a Comment