LIGI Kuu Tanzania Bara imeendelea tena leo kwa nyasi za viwanja vitatu tofauti kuwaka moto na kupatikana kwa matokeo tofauti. Katika mchezo uliochezwa jijini Dar es Salaam, Simba walikuwa wenyeji wa Ruvu Shooting katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Ikiwa ni mara ya kwanza kwa uwanja huo kutumika kwa mechi za ligi toka ulipofungwa kwa ajili ya matengenezo, Simba walianza vyema kwa kuitandika Ruvu kwa mabao 2-1 ambayo yalifungwa na Ibrahim Ajib na Mavugo. Kwingineko Yanga ya Dar es Salaam wakiwa wageni wa Ndanda FC ya Mtwara walijikuta waking’ang’aniwa kwa kwenda sare ya bila kufungana katika mchezo ulofanyika katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona. Huo Mbeya Azam FC ambao walikuwa wageni wa Tanzania Prison waliibuka kidedea kwa ushindi kiduchu wa bao 1-0 ambalo lilifungwa na Wilfried Balou dakika ya 60 kwenye mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Sokoine. Michuano hiyo itaendelea tena mwishoni mwa wiki hii ambapo viwanja nane tofauti vitawaka moto katika muendelezo wa ligi hiyo. Siku ya Jumamosi jijini Dar es Salaam, Yanga wataikaribisha Majimaji ya Songea katika Uwanja wa Uhuru, Ruvu Shooting watakabiliana na JKT Ruvu katika Uwanja wa Mabatini huko Mlandizi, Tanzania Prisons itaivaa Toto Afrika katika Uwanja wa Sokoine na Ndanda FC itavaana na Kagera Sugar katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona. Mechi zitakuwa zitakuwa ni Mbeya City dhidi ya Azam FC katika Uwanja wa Sokoine, Mwadui FC dhidi ya Stand United katika Uwanja wa Mwadui Complex huku Simba nao wakiikaribisha Mtibwa Sugar katika Uwanja wa taifa Dar es Salaam siku ya Jumapili.

No comments:
Post a Comment