Wednesday, September 21, 2016

KLOPP AWAPA TANO WACHEZAJI WAKE.



MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amepongeza ushindi wa mabao 3-0 waliopata katika mchezo wa mzunguko wa tatu wa Kombe la Ligi dhidi ya Derby County jana usiku lakini amesisitiza kuwa bado kuna nafasi ya kuimarika zaidi. Liverpool wametinga hatua ya 16 bora ya michuano hiyo kwa mabao yaliyofungwa na Ragnar Klavan, Philippe Coutinho na Divock Origi katika mchezo uliofanyika katika Uwanaj wa iPro. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Klopp alikipongeza kikosi chake kwa uwezo mkubwa walioonyesha na kuamini kuwa wanaweza kuimarika zaidi ya ilivyo hivi sasa. Klopp amesema walikuwa bora na walistahili kushinda kwa jinsi walivyotengeneza nafasi kufunga na kuzitumia. Pamoja na ushindi huo Klopp anaamini bado kuna mapungufu kadhaa ya kufanyia kazi ili waweze kuimarika zaidi.

No comments:

Post a Comment