Wednesday, September 21, 2016

CONTE AKATAA KUMUHAKIKISHIA FABREGAS.



MENEJA wa Chelsea, Antonio Conte amesifu mabao mawili yaliyofungwa na Cesc Fabregas lakini amesisitiza sifa hizo hazimaanishi chochote baada ya kutoka nyuma na kuichapa Leicester City jana. Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania alifunga mabao hayo katika muda wa nyongeza baada ya timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 katika muda wa kawaida katika mchezo huo wa mzunguko wa tatu wa Kombe la Ligi na kuwafanya kuibuka na ushindi wa mabao 4-2. Fabregas bado hajapata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu chini ya Conte huku mchezo pekee mwingine alioanza ulikuwa ni ule wa Kombe la Ligi dhidi ya Bristol City mwezi uliopita. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Conte amesema anataka ushindi na chaguo la kikosi chake hufanyika ili kupata ushindi na huwa hajali majina yao. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa kwa upande wake jambo muhimu wakati anapomwita mchezaji ni kumuonyesha kuwa hajafanya kosa kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment