Wednesday, September 21, 2016

WENGER AMMWAGIA SIFA PEREZ.



MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amependa alichokiona kutoka kwa mshambuliaji wake mpya Lucas Perez katika ushindi waliopata katika mchezo wa Kombe la Ligi dhidi ya Nottingham Forest jana. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania alifunga mabao yake mawili ya kwanza katika klabu kwenye ushindi wa mabao 4-0 iliyopata Arsenal jana. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Wenger alimsifu mshambuliaji huyo kwa kiwango kikubwa alichoonyesha haswa bao la pili alilofunga. Wenger amesema bao la pili alilofunga Perez limeonyesha ubora wake kiufundi, nia na morali ya kupambana.

No comments:

Post a Comment