Thursday, September 15, 2016

LEGIA WAOMBA RADHI KWA VURUGU ZA MASHABIKI WAO.

KLABU ya Legia Warsaw imeomba radhi kwa kelele za kunyanyapaa zilizokuwa zikipigwa na mashabiki wap na wanatarajia kuwapa adhabu wale wote waliohusika na vurugu hizo baada ya kuchapwa mabao 6-0 nd Borussia Dortmund jana. Taarifa zinadai kuwa mashabiki hao walizozana na watu wa usalama wakati wa mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na kujaribu kupenya ili kuingia jukwaa la mashabiki wageni. Legia ilikanusha kuwepo kelele za kibaguzi kutoka kwa mashabiki wa nyumbani lakini waliomba radhi kwa wale ambao walikwazika kwa namna moja au nyingine. Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA linasubiri kupata taarifa za mchezo huo ambapo baadae itapitiwa na kamati ya nidhamu.


No comments:

Post a Comment