Thursday, September 15, 2016

UWANJA WA OLIMPIKI WA NSK ULIOPO JIJINI VIENNA, KUANDAA FAINALI YA CHAMPIONS LEAGUE 2018.

SHIRIKISHO la Soka la Ulaya-UEFA limethibitisha kuwa Kiev ndio utakuwa mji mwenyeji wa fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2018. Kamati ya utendaji ya shirikisho hilo iliyokuwa ikiongozwa na rais mpya aliyechaguliwa Aleksander Ceferin iliuchagua Uwanja wa NSK Olympiyskyi uliopo Kiev mji mkuu wa Ukraine kuwa mwenyeji wa fainali hiyo.  Uwanja wa Lillekula uliopo katika mji wa Tallinn nchini Estonia ndio utakuwa mwenyeji wa mchezo wa Super Cup ya UEFA Agosti 14 mwaka 2018. Katika hatua nyingine UEFA katika mkutano wao mkuu maalumu uliofanyika huko Athens, Theodore Theodoridis amethibitishwa kuwa katibu mkuu akichukua nafasi ya Gianni Infantino. Infantino ameachia wadhifa huo baada kushinda uchaguzi wa rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Februari mwaka huu.

No comments:

Post a Comment