KIUNGO mpya wa Chelsea, N’Golo Kante amefanunua jinsi gani alivyokataa ofa ya meneja wa Manchester United Jose Mourinho kwa ajili ya kujiunga na Chelsea kiangazi hiki. Nyota huyo alijiunga na Chelsea akitokea Leicester City kwa kitita cha paundi milioni 29, lakini ilikuwa baada ya kukataa kwenda kuichezea United. Akihojiwa Kante amesema lilikuwa ni jambo zuri Mourinho kumpigia, ingawa alishaonywa toka awali jinsi gani atakavyomshawishi. Kante aliendelea kudai kuwa alimsikiliza meneja huyo lakini wakati huo tayari alishafanya maamuzi kwamba aidha abaki Leicester au aende Chelsea. Kante amesema mpaka wakati huo mazungumzo kati yake na Chelsea yalishaanza na alishakuwa na imani na Antonio Conte.
No comments:
Post a Comment