Friday, September 2, 2016

NITAIMARIKA BOURNEMOUTH - WILSHERE.

KIUNGO wa Arsenal, Jack Wilshere ana matumaini kuwa kwenda kwake kwa mkopo Bournemouth kutamsaidia kukua kama mchezaji. Mustakabali wa Wilshere Emirates ulikuwa mashakani wakati dirisha la usajili likikaribia kufungwa baada ya kusumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara msimu uliopita. Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza pia alishuhudia ushindani wa namba ukiongezeka kufuatia kusajiliwa kwa Granit Xhaka kutoka Borussia Monchengladbach kiangazi na Mohamed Elneny kutoka Basel Januari. Ujio wao huo na kurejea kwa Santi Cazorla kukamaanisha kuwa Wilshere atakuwa akitumika kama mchezaji wa akiba katika msimu huu mpya. Nyota huyo aliruhusiwa kuondoka kwa mkopo ili aweze kupata muda wa kutosha wa kucheza na kurejea katika kiwango chake, ambapo yeye mwenyewe anaamini ataimarika vyema akiwa Bournemouth.

No comments:

Post a Comment