Friday, September 2, 2016

TITE AWAMWAGIA SIFA NEYMAR NA GAGRIEL BAADA YA BRAZIL KUSHINDA.


KOCHA mpya wa timu ya taifa ya Brazil, Tite amewapongeza wafungaji Neymar na Gabriel Jesus baada ya nchi hiyo kushinda mabao 3-0 dhidi ya Ecuador katika mechi ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia iliyochezwa leo Alfajiri. Huo unakuwa mchezo wa kwanza wa kimashindano kwa Tite toka ateuliwe kuchukua mikoba ya Dunga baada ya nchi hiyo kushindw akufanya vyema katika michuano ya Copa America iliyofanyika Juni mwaka huu. Akihojiwa Tite amewapongeza makocha Cuca, Marcelo Oliveira na Oswald de Oliveira ambao wamefanya kazi na Gabriel. Tite amesema anawashukuru makocha hao kwani wamefanya kazi nzuri kumuandaa Gabriel kuwa mchezaji aliyekamilika. Mbali na kumwagia sifa Grabriel, Tite pia alimsifu Neymar na kuongeza kuwa nyota huyo pia ni matunda mazuri kutoka kwa makocha wazawa waliomuandaa vyema wakai akiwa Santos. Brazil inatarajiwa kuvaana na Colombia katika mchezo wao utakaofuata Septemba 6 huko Manaus.

No comments:

Post a Comment