RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA, Michel Platini amepewa ruhusa ya kutoa hotuba katika mkutano wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika wiki hii, pamoja na kuwa amefungiwa kujisughulisha na masuala yeyote ya michezo. Platini mwenye umri wa miaka 61 raia wa Ufaransa, alikuwa kiongozi wa UEFA mpaka alipofungiwa kwa kuvunja sheria za maadili kwa kupokea malipo yasiyo halali. Katika mkutano huo, UEFA wanatarajia kuchagua rais mpya atakaechukua nafasi ya kiungo huyo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa. UEFA ndio walioomba ruhusa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kwa rais wake wa zamani kutoa hotuba yake ya mwisho kabla ya kuchaguliwa kwa mbadala wake.
No comments:
Post a Comment