Monday, September 12, 2016

BEKI MSENEGAL WA PALACE APATA AJALI MBAYA.

BEKI wa Crystal Palace, Pape Souare amekimbizwa hospitali kwa helikopta baada ya kupata ajali ya gari jijini London lakini majeruhi aliyopata sio ya kutishia maisha yake. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26, aliumia paja na taya katika ajali hiyo iliyotokea jana na anatarajiwa kuendelea kubakia hospitalia akipatiwa matibabu. Souare hakuwepo katika kikosi cha Palace kilichoitandika Middlesbrough kwa mabao 2-1 Jumamosi iliyopita. Katika taarifa iliyotolewa na klabu hiyo, ilithibitisha taarifa hizo na kudai wanafuatilia kwa karibu hali ya mchezaji huyo inavyoendelea na kutoa pole kwa familia yake. Nyota huyo wa klimataifa wa Senegal alijiunga na Palace akitokea Lille ya Ufaransa Januari mwaka 2015, na mara ya mwisho kuichezea Palace ilikuwa katika mchezo dhidi ya Bournemouth Agosti 27 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment