Saturday, September 24, 2016

POGBA AONA MWEZI WAKATI MAN UNITED ILIPOIDHALILISHA LEICESTER.



KLABU ya Manchester United imerejesha makali yake ya ushindi katika Ligi Kuu kwa kuwachapa mabingwa Leicester City kwa mabao 4-1 katika Uwanja wa Old Trafford. Nahodha Wayne Rooney aliachwa katika benchi kwenye mchezo huo ambao Chris Smalling alifunga bao la kwanza dakika ya 22 kabla ya Juan Mata hajaongeza la pili dakika ya 37. Muda mchache baadae Mata akaja kutengeneza bao safi lilifungwa na Marcus Rashford dakika ya 40 na Paul Pogba alipigilia msumari wa mwisho kwa kufunga bao lake la kwanza kwa klabu hiyo dakika ya 42. Kipindi cha pili Leicester walijitahidi kurejea mchezoni na kufanikiwa kupata bao la kufutia machozi dakika ya 59 kupitia kwa Demarai Gray.

No comments:

Post a Comment