Friday, September 9, 2016

REAL MADRID, ATLETICO WAPOTEZA RUFANI ZAO.

KLABU za Real Madrid na Atletico Madrid zimepoteza rufani zao kupinga kufungiwa na Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA kusajili wachezaji katika vipindi viwili vya usajili. Klabu hizo zilikuwa zikipinga uamuzi huo wa FIFA kuwaadhibu kwa la kuvunja sheria za usajili kwa wachezaji wa kigeni wenye umri wa chini ya miaka 18. FIFA ilikuwa imetoa adhabu hiyo Januari mwaka huu, lakini rufani iliyokatwa ilizipa nafasi klabu hizo kuweza kusajili wachezaji kipindi hiki cha kiangazi. Baada ya rufani yao kukataliwa FIFA sasa klabu hizo zinategemea kupeleka rufani yao katika Mahakama ya Michezo ya Kimataifa-CAS.

No comments:

Post a Comment