Friday, September 9, 2016

WENGER AMTABIRIA MAKUBWA WILSHERE ARSENAL.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amedai kuwa Jack Wilshere anaweza kuitumikia klabu hiyo kw akipindi kirefu huko mbele na kusisitiza kuwa kiungo huyo hana chochote cha kumuonyesha zaidi ya kuwa fiti. Wilshere amekwenda kwa mkopo wa msimu mzima Bournemouth dakika za mwisho kabla ya dirisha la usajili majira ya kiangazi halijafungwa ikiwa kama sehemu ya mikakati ya kujijenga upya kufuatia kusumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara katika misimu miwili iliyopita. Akizungumza kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Southampton, Wenger alipuuza habari kuwa amekuwa haelewani na kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye amekuwa akimtaja kuwa na uwezo mkubwa. Wenger amesema alizungumza na Wilshere nay eye mwenyewe alimwambia hadhani kama ataweza kupata muda wa kutosha kucheza akibakia hapo kwasababu anadhani anataka kucheza zaidi msimu huu baada ya kupona majeruhi. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa alimruhusu kuondoka kwasababu alikuwa hawezi kumuahidi muda wa kutosha wa kucheza kama alivyotaka mwenyewe.

No comments:

Post a Comment