Friday, September 9, 2016

NEYMAR ILIBAKI KIDOGO AJIUNGE NA KATI YA PSG AU MAN UNITED - WAKALA.

WAKALA wa mshambuliaji wa Barcelona, Neymar amedai kuwa mteja wake huyo alikaribia kujiunga na Paris Saint-Germain na Manchester United katika usajili wa majira ya kiangazi kabla ya hatimaye kuamua kuongeza mkataba wake katika klabu hiyo. Neymar mwenye umri wa miaka 24, aliongeza mkataba wake Barcelona ambao utamalizika mwaka 2021, lakini wakala wake Wagner Ribeiro amebainisha kuwa uhamisho wa hela nyingi kwenda kwingineko ulijadiliwa. Akihojiwa Ribeiro amesema Neymar alibakia kidogo ajiunge na PSG na kama hilo lingefanikiwa angeweza kukunja kitita cha euro milioni 40 kwa mwaka. Wakala huyo pia aliongeza United nao walitaka saini ya nyota huyo lakini aliamua kuongeza mkataba wake kwakuwa alitaka kubakia Barcelona. Kama mabingwa hao wa Ufaransa wakimuhitaji Neymar siku za usoni itabidi waongeze fedha kwani kitenzi katika mkataba hivi sasa kimefikia euro milioni 200 kwa klabu itakayomuhitaji huku kikizidi kukua na kufikia euro milioni 250 kufikia mwaka 2019.

No comments:

Post a Comment