MENEJA wa Crystal Palace, Alan Pardew amedai kuwa beki wa Crystal Palace, Pape Souare anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi sita baada ya baada ya kuvunjika mfupa wa paja katika ajali ya gari aliyopata. Nyota huyo wa kimaaifa wa Senegal mwenye umri wa miaka 26, alikimbizwa hospitali kwa helikopta baada ya ajali hiyo aliyopata Jumapili iliyopita jijini London. Majeruhi pia yanamaanisha atakosa michuano ya Mataifa ya Afrika itakayofanyika Januari mwakani. Akihojiwa Pardew amesema beki huyo hayupo katika wakati mzuri lakini watu wote wako pamoja naye wakimuunga mkono katika kipindi hiki kigumu. Souare anategemewa kuachiwa kutoka Hospitali Jumamosi hii.
No comments:
Post a Comment