MENEJA wa Atletico Madrid, Diego Simeone amethibitisha kuwa mkataba wake na klabu hiyo ya La Liga ulipunguzwa kwa miaka miwili kiangazi mwaka jana, lakini amesisitiza kuwa hakuna chochote kilichobadilika. Taarifa zilibainisha mapema wiki hii kuwa, baada ya mazungumzo kufuatia Atletico kupoteza fainali ya pili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika kipindi cha miaka mitatu, Simeone alikubaliana na wamiliki wa klabu hiyo kwa mkataba wake sasa kuishia Juni mwaka 2018. Akihojiwa kufuatia kuvuja kwa taarifa hizo, Simeone alikiri kuwa ni kweli suala hilo lilitokea lakini hakuna lililobadilika kwani anafurahia mahali alipo. Meneja huyo amesema haoni kama kuna tatizo kwenye hilo suala kwani katika kipindi cha miaka miwili anaweza kusaini mkataba mwingine mpya kama wamiliki wakiwa bado wanahitaji huduma yake.
No comments:
Post a Comment