Friday, September 16, 2016

AGUERO KUONGEZA MKATABA MAN CITY.

MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Sergio Aguero anadaiwa kukubali kuongeza mkataba wa mwaka mmoja zaidi ambao utamuweka katika klabu hiyi mpaka mwaka 2020. Aguero mwenye umri wa miaka 28, amewahi kusema atajiunga tena na klabu yake ya kwanza ya Independiente pindi atakapomaliza mkataba wake mwaka 2019. Hata hivyo, nyota huyo wa kimataifa wa Argentina sasa anaonekana ataendelea kubakia Etihad kwa mwaka mmoja zaidi. Aguero ameanza msimu huu kwa kiwango cha juu, akiwa amefunga mabao tisa katika mechi tano zikiwemo hat-trick katika mechi mbili za michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Akihojiwa Aguero amesema anategemea kufunga mabao zaidi chini ya meneja mpya Pep Guardiola kwani ni meneja anayefurahia aina ya mchezo wake. Aguero alijiunga na City akitokea Atletico Madrid mwaka 2011 kwa kitita cha paundi milioni 38 na ameshafunga mabao 145 katika mechi 213 alizoichezea City.

No comments:

Post a Comment