Friday, September 16, 2016

KLOPP ATAMBIA WASHAMBULIAJI ALIONAO.

MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema isingewezekana kuimarisha safu yake ya ushambuliaji katika kipindi cha usajili wa kiangazi kwakuwa kulikuwa hakuna mshambuliaji ambaye alikuwa bora zaidi ya wale alionao. Liverpool imefunga mabao 50 katika Ligi Kuu mwaka huu zaidi ya timu yeyote na kuongezeka kwa Sadio Mane aliyetoka Southampton kwa kitita cha paundi milioni 30 Juni kumeimarisha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo zaidi ya ilivyokuwa awali. Vijana wa Klopp wamefunga mabao manne katika mchezo dhidi ya Arsenal na mabingwa Leicester City mpaka sasa msimu huu na Klopp ameisifu safu yake ya ushambuliaji kwa uwezo mkubwa walioonyesha. Akihojiwa Klopp amesema kiangazi watu wengi walikuwa wakitaka asajili washambuliaji zaidi lakini ukweli ni kuwa hakupata mshambuliaji ambaye alikuwa bora zaidi ya wale aliokuwa nao.

No comments:

Post a Comment