MSHAMBULIAJI nyota wa Manchester City, Sergio Aguero amebainisha kuwa meneja wao Pep Guardiola alimwambia kuwa alitaka kuja kuifundisha timu ya taifa ya Argentina. Aguero anafanya kazi na meneja huyo wa zamani wa Barcelona kwa mara ya kwanza msimu huu kufuatia kuondoka Manuel Pellegrini. Lakini nyota huyo amebainisha kuwa angeweza kukutana na Guardiola mapema zaidi kama angepata kazi hiyo. Aguero amesema aliwahi kuzungumza na Guardiola kuhusu timu ya taifa na alidai kuwa kama Argentina wangempigia mapema angeweza kwenda kuwafundisha kwani anakipenda kikosi chao.
No comments:
Post a Comment