Wednesday, October 12, 2016

KOCHA WA ALGERIA AJIUZULU KUFUATIA SARE.

KOCHA wa timu ya taifa ya Algeria, Milovan Rajevac amejiuzulu wadhifa wake huo baada ya kuisimamia timu hiyo katika mechi mbili pekee. Uamuzi wake unafuatia sare ya bao 1-1 aliyopata nyumbani dhidi ya Cameroon Jumapili iliyopita katika mchezo wa kundu F wa kufuzu Kombe la Dunia. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 62 raia wa Serbia alikutana na rais wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo Mohamed Raouraoua jana kujadili matokeo na kuondoka kwake kulitangazwa muda mfupi baada ya mazungumzo hayo. Rajevac alichukua mikoba ya Mfaransa Christian Gourcuff ambaye aliacha kibarua hicho Aprili mwaka huu.

No comments:

Post a Comment