Wednesday, October 19, 2016

MATOKEO YA LIGI KUU YAMNYIMA RAHA RANIERI.



MENEJA wa Leicester City, Claudio Ranieri amesisitiza bado ana hasira na kikosi chake pamoja na kufanikiwa kupiga hatua kubwa kuelekea hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Bao pekee la Riyad Mahrez lilitosha kuipa ushindi wa bao 1-0 Leicester dhidi ya FC Copenhagen ya Denmark na kuendelea rekodi yao ya ushindi wa asilimia 100 Ulaya na kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa kundi G. Kama wakifanikiwa kupata ushindi katika mchezo wao wa marudiano dhidi ya Copenhagen Novemba 2, moja kwa moja watakuwa wametinga hatua hiyo baada ya kuwa tayari wameshawafunga Club Brugge na FC Porto. Leicester wamepata alama nyingi zaidi katika mechi tatu za Ligi ya Mabingwa Ulaya kuliko mechi nane za Ligi Kuu walizocheza na Ranieri amekiri kutofurahishwa na hali inavyoendelea. Ranieri anafurahia kwa upande mmoja lakini upande anachukizwa kutokana na hali ilivyo kwani katika mechi nane za ligi wameambulia alama nane pekee.

No comments:

Post a Comment