MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola amekiri alijaribu kumsajili kipa wa Barcelona Marc-Ander ter Stegen majira ya kiangazi kabla ya kuamua kumchukua Claudio Bravo. Lakini Guardiola amekanusha taarifa kuwa alijaribu kuwachukua wachezaji wake wanne wa zamani wa Barcelona na kuwaleta Etihad akiwemo Lionel Messi. Guardiola alikuwa akihitaji kipa mpya City ambaye anaweza kucheza vyema mipira ya miguu na alikwenda Camp Nou ambako walikuwa Ter Stegen na Bravo waliokuwa wakishirkiana katika majukumu ya kipa namba moja. Akihojiwa Guardiola amesema alifahamu kuwa Ter Stegen alikuwa akitaka kucheza wakati wote hivyo aliwasiliana naye lakini iliposhindikana ndio maana alihamia kwa Bravo kwani wote wawili wanashabihiana. Meneja huyo amesisitiza kuwa kamwe hakujaribu kumsajili yeyote zaidi kutoka katika klabu hiyo ambayo ameifundisha kwa miaka minne.
No comments:
Post a Comment