CHAMA cha Soka cha Misri-EFA kimetangaza kuwa kitaruhusu mashabiki 50,000 kuhudhuria mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia kati ya Misri na Ghana utakaofanyika jijini Alexandria. Mchezo huo unatarajiwa kufanyika Jumapili ya Novemba 13 katika Uwanja wa Borg El Arab. Kuzuiwa kwa mashabiki katika mechi nchini humo kuliwekwa toka mwaka 2012 wakati mashabiki 72 wa Al Ahly walipokufa kufuatia vurugu zilizotokea huko Port Said. EFA pia imetangaza kuwa mashabiki 40,000 wataruhusiwa kwnda kuangalia mchezo wa fainali ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo itafanyika jijini Alexadria. Katika mchezo huo Zamalek watakuwa wenyeji wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini Jumapili hii.
No comments:
Post a Comment