Monday, October 3, 2016

SWANSEA YAMTIMUA KOCHA WAKE.

KLABU ya Swansea City imemtimua meneja wake Francesco Guidolin na nafasi kuchukuliwa na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Marekani Bob Bradley. Swansea hawajashinda mechi yeyote ya Ligi Kuu toka kuanza kwa msimu na sasa wanashika nafasi ya 17 katika msimamo. Bradley ambaye pia amewahi kuzifundisha Misri na klabu ya Stabaek ya Norway, anaiacha timu ya Le Havre inayoshiriki ligi daraja la pili Ufaransa na kwenda kuchukua nafasi ya Guidolin aliyeteuliwa Januari mwaka huu. Viongozi wa klabu hiyo wanadaiwa kuzungumza na makocha kadhaa kwa ajili ya nafasi hiyo akiwemo nahodha wa zamani wa kimataifa wa Wales Ryan Giggs. Kibarua cha kwanza cha Bradley mwenye umri wa miaka 58, kitakuwa kusimamia mchezo dhidi ya Arsenal Octoba 15 mwaka huu baada ya mapumziko kupisha mechi za kimataifa kumalizika.

No comments:

Post a Comment