Monday, October 3, 2016

ARMENIA WABAINISHA KULICHOMSIBU MKHITARYAN.

IMEBAINIKA kuwa kiungo Henrikh Mkhitaryan alikosa mchezo wa Manchester United waliotoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Stoke City kutokana na majeruhi ya nyonga na klabu yake imetuma barua ya kuomba kuenguliwa kwa nyota huyo katika kikosi cha Armenia. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 ameanza katika mechi pekee toka aliposajiliwa akitokea Borussia Dortmund Julai mwaka huu na hajacheza toka walipofungwa na Manchester City Septemba 10. Kulikuwa na matumaini ya nyota huyo kurejea katika mchezo wa jana baada ya kutuma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kuwa ameanza mazoezi na anakaribia kuwa fiti lakini kwa mara nyingine alikosekana. Armenia walitoa barua waliyotumiwa na daktari wa United Steve McNally ambaye inaelezea hali ya Mkhitaryan ilivyo na pia kuomba aondolewe katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia za nchi hiyo. Armenia wataanzia nyumbani kucheza na Romania Jumamosi hii kwenye mchezo wa kundi E kabla ya kusafiri kuifuata Poland Jumanne ya wiki inayofuata.

No comments:

Post a Comment