Wednesday, November 23, 2016

BAADA YA KUFUZU CHAMPIONS LEAGUE LEICESTER SASA NGUVU ZOTE LIGI KUU.

MENEJA wa Leicester City, Claudio Ranieri amedai kuwa kikosi chake sasa kinapaswa kuhamishia ubora wao walioonyesha katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenda katika Ligi Kuu. Leicester walifuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo huku wakiwa wamebaki na mechi moja mkononi ka kuitandika Club Brugge ya Ubelgiji kwa mabao 2-1 jana. Lakini pamoja na kufanya vyema Ulaya hali imekuwa tofauti nyumbani kufuatia kupoteza mechi sita kati ya 12 za Ligi Kuu walizocheza msimu huu huku wakishika nafasi ya 14. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Ranieri amesema kuwa sasa mawazo yao yanahamia katika Ligi Kuu. Leicester walikwenda katika mchezo huo wakihitaji alama moja ili wafuzu lakini walifanikiwa kuondoka na alama zote tatu na kuongoza kundi G.

No comments:

Post a Comment