KLABU za Chelsea na Tottenham Hotspurs zinadaiwa kupitwa na Bayern Munich katika kinyang’anyiro cha kumuwania kiungo wa Real Madrid Isco. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania amekuwa akizivuia klabu za Ligi Kuu kwa kipindi kirefu huku Chelsea na Spurs zikitajwa kama timu zinamtaka. Kushindwa kwa Madrid kumpatia mkataba mpya Isco kumesaidia kufungua milango kwa kiungo kuondoka wakati dirisha la usajili wa Januari likikaribia. Taarifa zinadai kuwa Bayern wako tayari kutoa kiasi kikubwa cha fedha kuzidi klabu hizo za Uingereza zinazomuwania.
No comments:
Post a Comment