Tuesday, November 15, 2016

CHELSEA YATAKA KUMPA KIBARUA LAMPARD AKISTAAFU.

KLABU ya Chelsea inadaiwa kujipanga kumpa kibarua Frank Lampard pindi atakapoamua kustaafu soka lake. Mapema jana Lampard alitangaza kuwa ataondoka katika timu ya New York City FC wakati mkataba wake utakapomalizika mwezi ujao. Kiungo huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 38 amesema atatangaza uamuzi wake mapema kama atastaafu soka lakini taarifa zinadai kuwa Chelsea wako tayari kumpa nafasi Stamford Bridge. Lampard amewahi kuitumikia Chelsea kwa kipindi cha miaka 13 akifunga mabao 211 katika mechi 648 alizocheza na kushinda mataji matatu ya Ligi Kuu. Mkongwe huyo aliondoka Chelsea mwaka 2014 baada ya kukubali kujiunga na klabu hiyo ya Marekani.

No comments:

Post a Comment