KLABU ya Real Madrid imepata taarifa nzuri za majeruhi wake wakati wakielekea katika mchezo wao dhidi ya mahasimu wao Atletico Madrid mwishoni mwa wiki hii kufuatia Sergio Ramos kuanza mazoezi baaa ya kukaa nje kwa muda kutokana na maumivu ya goti. Mara ya mwisho kwa beki huyo kuichezea Madrid ilikuwa katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Dortmund ambao walitoka sare ya mabao 2-2 Septemba 27 mwaka huu. Lakini sasa inaonekana ameweza kupona kwa wakati tayari kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya Atletico baada ya kufanya mazoezi jana na wenzake. Beki mwingine wa Madrid Pepe ambaye anasumbuliwa na matatizo ya msuli wa paja bado hajaanza mazoezi na wachezaji wenzake sambamba na Karim benzema na Casemiro.
Tuesday, November 15, 2016
RAMOS ATOA MATUMAINI KWA MADRID.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment