BEKI mkongwe wa kimataifa wa Ivory Coast, Kolo Toure amependekeza kaka yake Yaya Toure aondoke Manchester City na kwenda kuanza upya katika klabu ya Marseille ya Ufaransa. Yaya Toure mwenye umri wa miaka 33 hajacheza mechi yeyote ya Ligi Kuu msimu huu akiwa na City baada ya kauli ya wakala wake iliyomuudhi meneja wake Pep Guardiola. Kiungo huyo aliomba radhi wiki iliyopita akitimiza matakwa ya Guardiola ili aweze kuitwa tena katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Lakini kaka yake Kolo ambaye kwasasa anacheza katika klabu ya Celtic ya Scotland amesema anadhani Marseille itakuwa sehemu sahihi kwa ndugu yake huyo kutokana na mipango yao. Kolo Toure amesema hajazungumza naye kuhusu suala hilo kwakuwa anafahamu bado yuko City na anaheshimu hilo lakini anadhani Marseille ni klabu kubwa na Yaya analifahamu vyema soka la Ufaransa.

No comments:
Post a Comment