Tuesday, November 15, 2016

PIGO KUBWA HULL CITY.

MSHAMBULIAJI wa Hull City, Will Keane anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa miezi 12 kufuatia kuumia goti. Keane mwenye umri wa miaka 23 alipata majeruhi hayo katika ushindi wa mabao 2-1 waliopata dhidi ya Southampton Novemba 6 mwaka huu kabla ya kufanyiwa upasuaji mapema leo. Nyota huyo alijiunga na Hull City akitokea Manchester United Agosti 30 mwaka huu na tayari ameshacheza mechi sita msimu huu. KLabu hiyo ilithibitisha taarifa kupitia mtandao wake na kudai kuwa ni pengo kubwa kumkosa mchezaji huyo kwa kipindi chote hicho. Hull kwasasa wanashikilia nafasi ya 18 katika msimamo wa Ligi Kuu wakiwa alama moja nyuma ya West Ham United wanaoshikilia nafasi ya 17.

No comments:

Post a Comment