Tuesday, November 15, 2016

UNITED YATAJWA KUMUWANIA CHIPUKIZI WA PORTO.

KLABU ya Manchester United inadaiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha kumuwania mshambuliaji wa Fc Porto Andre Silva. Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 21, amekuwa katika kiwango juu katika mechi za nyumbani na Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu huku akiwa amefunga mabao manne katika mechi tano za kikosi cha timu ya taifa ya Ureno alizocheza. Barcelona, Real Madrid na Manchester Cit nazo pia zimetajwa kumfuatilia kwa karibu chipukizi huyo. Hata hivyo, Silva anadaiwa hatakuwa rahisi kwani United na klabu zingine kubwa zinazomuwania zitatakiwa kulipa kitita cha euro milioni 60 ili kutengua kitenzi katika mkataba wake mpya aliosaini na Porto hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment