Friday, November 11, 2016

FIFA YAIRUKA UINGEREZA.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limedai kuwa halijafungia wachezaji wa Uingereza na Scotland kuvaa viua maalumu, na kusisitiza madai yote kuhusiana na suala hilo ni kupotosha ukweli. Timu zote Uingereza na Scotland zimeambiwa zivae beji nyeusi mikononi zenye nembo ya viua katika mchezo wao wa kufuzu Kombe la Dunia baadae leo ili kukumbuka mashujaa wao waliopoteza maisha katika vita. Sheria inakataza kwa timu yeyote kuvaa nembo yenye ujumbe wa kisiasa katika fulana zao na FIFA imesema hawana mamlaka yeyote ya kutengua sheria hiyo. Timu za Ireland ya Kaskazini na Wales ambazo zipo chini ya koloni la Uingereza zinatarajiwa kuvaa beji nyeusi pekee mikononi kwa madai kuwa FIFA waliwakataza kuweka viua hivyo katika fulana zao. Hata hivyo FIFA ilikanusha taarifa hizo na kudai kuwa timu hizo zilipoomba kufanya hivyo walikumbushwa sheria inatakaje na sio vinginevyo.

No comments:

Post a Comment