KIPA wa timu ya taifa ya Chile, Claudio Bravo amepata majeruhi yaliyomfanya kutolewa nje katika sare ya bila kufunga iliyopata nchi yake dhidi ya Colombia katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia uliofanyika huko Baranquilla jana. Bravo aliumia mguu wake wa kulia wakati wakiwa katika harakati ya kuokoa hatari langoni mwake, alitibiwa uwanjani lakini baada ya muda alitolewa nje baada ya kuonekana bado ana maumivu. Nafasi ya kipa huyo anayekipiga katika klabu ya Manchester City ilichukuliwa na Johnny Herrera. Hata hivyo, kocha wa timu hiyo Antonio Pizzi amesema kuwa nadhani Bravo atapona kwa wakati kwa ajili ya mchezo wao ujao wa kufuzu dhidi ya Uruguay Jumanne ijayo.
No comments:
Post a Comment