Monday, November 21, 2016

HOENESS AUTAKA TENA URAIS BAYERN.

RAIS wa zamani wa Bayern Munich, Uli Hoeness amesisitiza kuwa hawezi kukaa mbali na klabu hiyo wakati akijiandaa kuiwinda tena nafasi yake ya urais kwa mabingwa hao wa Bundesliga. Hoeness alilazimika kuachia ngazi mwaka 2014 wakati akitumikia adhabu ya kifungo jela kwa kosa la kukwepa kodi lakini bado ameendelea kupigiwa upatu wa kuingoza tena klabu hiyo. Nguli huyo wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani alidai kuwa anafurahia kuungwa mkono na wafanyakazi wote w Bayern na mke wake katika hatua zake za kuitaka tena nafasi hiyo. Hoeness alidai kuwa aliiomba familia yake kugombea tena nafasi hiyo na wakamkubalia kwani wanafahamu furaha yake ni kuiongoza klabu hiyo anayoipenda.

No comments:

Post a Comment