MSHAMBULIAJI nyota wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic anatarajiwa kutengenezewa sanamu kwa heshima yake baada ya kutajwa mchezaji bora wa Sweden kwa miaka 10 mfululizo. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 36 alitwaa tuzo hiyo ya Mpira wa Dhahabu jana katika sherehe zilizofanyika jijini Stockholm. Sanamu hilo linatarajiwa kukaa nje ya Uwanja wa Friends Arena uliopo Stockholm ambako Ibrahimovic alifunga mabao manne katika mchezo dhidi ya Uingereza mwaka 2012. Akihojiwa Ibrahimovic amesema jambo hilo ni kubwa sana kwake kwani watu wengi huwa hawapati heshima ya kutengenezewa sanamu mpaka wanafariki dunia. Ibrahimovic ambaye alistaafu soka la kimataifa baada ya michuano ya Ulaya mwaka huu, amefunga mabao 62 katika mechi 116 alizochezea Sweden huku akishinda mataji la ligi katika nchi nne tofauti.
No comments:
Post a Comment