Friday, November 18, 2016

KOSCIELNY KUONGEZA MKATABA ARSENAL.

BEKI wa Arsenal, Laurent Koscielny anadaiwa kukaribia kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa alijiunga na Arsenal mwaka 2010 akitokea Lorient na toka kipindi hicho ameimarika na kuwa mchezaji tegemeo wa timu hiyo. Arsenal inataka kumuongeza mkataba wa muda mrefu na taarifa zinadai kuwa tayari wameshafikia makubaliano ya kumuongeza mkataba mpaka mwaka 2020. Mkataba wa sasa wa beki huyo unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu na mkataba wake mpya unatarajiwa kutangazwa kabla ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint-Germain Jumatano ijayo.

No comments:

Post a Comment