MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Danny Ings anatarajiwa kukaa nje kwa zaidi ya miezi tisa kufuatia majeruhi ya goti ambayo yatamlazimu kufanyiwa upasuaji. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, alipata majeruhi hayo katika goti lake la mguu wa kulia wiki iliyopita kwenye mchezo wa Kombe la Ligi dhidi ya Tottenham Hotspurs. Akihojiwa meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp alithibitisha taarifa hizo na kuongeza kuwa ana matumaini nyota huyo atarejea akiwa imara zaidi. Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wiki hii jijini London. Ings alijiunga na Liverpool akitokea Burnley Juni mwaka 2015 kwa ada ya paundi milioni nane.
No comments:
Post a Comment