MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Eden Hazard amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Octoba wa Ligi Kuu. Hazard ambaye amabadilika kwa kiasi kikubwa toka Chelsea ilipochukuliwa na Antonio Conte, amechaguliwa kutwaa tuzo hiyo na Chama cha Wachezaji Kulipwa-PFA. Nyota huyo amefunga mabao matatu na kutengeneza lingine moja katika mechi nne alizocheza mwezi uliopita, na kuisaidia Chelsea kukaa katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi. Hazard ameshinda kwa kura 27,262 na kumzidi winga wa Arsenal Theo Walcott aliyepata kura 14,737. Nyota wa Stoke City Joe Allen, Dele Alli wa Tottenham Hotspurs na Charlie Austin wa Southampton pia walikuwepo katika kinyang’anyiro hicho sambasamba na mshambuliaji wa Bournemouth Callum Wilson.
No comments:
Post a Comment