Wednesday, November 2, 2016

WAZIRI MKUU WA UINGEREZA AIJIA JUU FIFA.

WAZIRI mkuu wa Uingereza, Theresa May amesema kukataa kwa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kuwaruhusu wachezaji wa wa Uingereza na Scotland kuvaa beji yenye mfano wa ua katika fulana zao ni jambo baya. Mataifa hayo mawili yanatarajiwa kukutana Novemba 11 mwaka huu, siku moja wakati nchi hiyo ikikumbuka mashujaa wake waliopoteza maisha katika vita. FIFA zimeshapiga marufuku ujumbe wowote unaoashiria masuala ya kisiasa, kidini au kibiashara katika fulana. May amesema FIFA wanapaswa kuliangalia suala hilo upya kwani wachezaji wanataka kutambua na kuheshimu wale wote waliopoteza maisha yao kwa ajili ya usalama wao.

No comments:

Post a Comment