OFISA mkuu wa Juventus, Beppe Marotta amekingia kifua malipo ya euro milioni 27 kama ada ya uwakilishi kwenda kwa wakala wa Paul Pogba, Mino Raiola kama sehemu ya usajili wa kiungo huyo kwenda Manchester United majira ya kiangazi. Raiola alipata kiasi hicho cha fedha wakati Pogba mwenye umri wa miaka 23 aliporejea United akitokea Juventus kwa ada iliyovunja rekodi ya dunia ya euro milioni 105 agosti mwaka huu. Marotta amesema kufuata na ukweli kuwa uhamisho wa nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa kuwa mkubwa katika historia ya soka hiyo inamaanisha na wakala wake lazima apate kitita kikubwa. Marotta aliendelea kudai kuwa kulingana na kiasi walichopewa na United kwa mchezaji huyo bado wametengeneza faida kubwa pamoja na kumlipa Raiola paundi milioni 27.

No comments:
Post a Comment