Monday, November 14, 2016

SANCHEZ AREJEA MAZOEZINI CHILE PAMOJA NA MAJERUHI.

MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Alexis Sanchez amerejea mazoezini na kikosi cha Chile pamoja na kuwa na majeruhi ya msuli na anaweza kujaribu kucheza katika mchezo wa katikati ya wiki wa kufuzu Kombe la Dunia bila ridhaa ya meneja wa klabu yake Arsenal Wenger. Sanchez alifanya mazoezi ya asubuhi na Chile Jumapili asubuhi huku mguu wake wa kulia ukiwa umefungwa bandeji kubwa baada ya kuumia akiwa mazoezini wiki iliyopita. Hata hivyo, Wenger amewaonya Chile dhidi ya kumtumia Sanchez na anataka kuhakikisha mshambuliaji huyo anakuwa fiti kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Manchester United kule Old Trafford mwishoni mwa wiki hii. Akihojiwa Wenger amesema wanapaswa kuzingatia afya ya Sanchez kwani kumchezesha huku akiwa majeruhi ni hatari kwasababu anaweza kukaa nje kwa kipindi kirefu zaidi.

No comments:

Post a Comment