Monday, November 14, 2016

HARRY KANE MGUU NJE MGUU NDANI SPURS.

MSHAMBULIAJI nyota wa Tottenham Hotspurs, Harry Kane anaweza kuondoka kufuatia klabu hiyo kukataa kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi White Hart Lane. Nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza kwasasa analipwa kitita cha paundi 60,000 kwa wiki, lakini anataka kuongezwa mshahara wake na kuwa mchezaji anayelpwa zaidi katika klabu hiyo. Kama majadiliano hayo yaklishindikana, Kane mwenye umri wa miaka 23 anaweza kuondoka huku klabu za Chelsea, Manchester City na Manchester United zikidaiwa kuitamani saini yake. Msimu huu Kane amefunga mabao matatu klatika mechi sita za Ligi Kuu walizocheza.

No comments:

Post a Comment